Chama cha KANU katika eneo la Lurambi kinaomboleza kifo cha mzee  Peter Andayi  kutoka wadi ya Butsotso Mashariki ambaye amekuwa msingi wa chama hicho kwa zaidi ya miaka thelathini na mitano ambaye amefariki kifo cha ghafla kutokana na mshtuko wa moyo

Wanachama wa kanu ambao waliitembelea familia ya mzee andayi  kata ndogo ya Emurumba Butsotso Mashariki wakiongozwa na Alfred Muyeshi wamesema kifo hicho cha ghafla ni pigo kubwa kwa chama cha KANU na hata baraza la tamaduni za jamii ya watoto ambapo amekuwa mshauri.

Familia ikiongozwa na kasisi David Andayi ambaye pia ni kiongozi wa makanisa ya PEFA Lurambi Kaskazini wanasema mzee alishtuka na kuzimia na kudhibitishwa kuwa amefariki baada kufikishwa hospitali ya Mukumu

By Linda Adhiambo

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE