Huzuni imetanda katika eneo la Kabula kaunti ya Bungoma baada ya mwanafuzi wa kidato cha pili kujitia kitanzi kufuatia ugomvi na wazazi wake kwa makataa ya kuenda shule

Joan Wekesa  ambaye alikuwa mwanafunzi katika shule ya upili ya Naburereya aLijitia kitanzi asubuhi ya Jumatatu akiwa ndani ya  nyumba ya mpenzi wake anayeishi karibu na soko la Kabula.

Wekesa alikuwa amemtembelea mpenziwe siku ya Jumapili na kulala kwake, jambo ambalo halikuridhisha mama yake aliyefika pale siku iliyofuata na kumwagiza aende shule.

Praxidese Wekesa  ambaye ni mama ya marehemu alisema kuwa juhudi zake za kujaribu kumshawishi bintiye akubali kuenda kusoma ziliangulia patupu na hapo akaamua kuenda kumuita mumewe ili wasaidiane kumrejesha mtoto wao shuleni.

Praxidese alisema kuwa bintiye alikuwa amekataa kabisa kurejea shuleni huku  akitishia kujinyonga iwapo angeendelea kumshawishi ili arudi shuleni.

Alisema kwamba hakuamini Joan angetekeleza vitisho vyake vya kujinyonga na  kudai kuwa alishtuka sana aliporudi pale na kupata mwili wa mtoto wake ukining’inia kwenye kamba.

Tukio hilo limethibitishwa na naibu chifu wa eneo hilo na mwili wa marehemu umepelekwa katika chumba cha kuifadhi wafu cha hospitali ya Bungoma

By Lihavi Imelda

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE