Familia moja katika kijiji cha mukama kata ndogo ya kochwa eneo bunge la navakholo inaomboleza kifo cha mwanao mwenye umri wa miaka 19 mwanafunzi wa darasa la saba katika shule ya msingi ya Mukama baada ya kunywa sumu kwa madai ya kulazimishwa kwenda shule 

Kulingana na jefnea munyasa babake marehemu kwa jina job mavale  inadaiwa kuchukua hatua ya kujitoa uhai kwa kunywa dawa ya kuwauwa kupe baada ya kushinikizwa kwa siku tatu mfululizo kwenda shuleni zilipofunguliwa kufuatia agizo la serikali kuamuru wanafunzi wote warudi shuleni

Mamake hellen munyasa ambaye aliyempata mwanawe chooni baada ya kunywa sumu anasema  mwanawe alikuwa amejiingiza kwenye mihadarati na unywaji wa pombe wakati wa likizo ya korona na imechangia pakubwa kwake kususia shuleni

Sasa wakazi wanaitaka serikali kubuni njia mwafaka ya kutekeleza agizo la kurejeshwa wanafunzi shuleni pasi na kuwashurutisha kabla ya kupewa ushauri nasaha

Story by Richard Milimu

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE