Familia moja kutoka mtaa wa Shikhambi wadi ya Shieywe viungani mwa mji wa Kakamega inaishi kwa hofu baada ya mwanaume mmoja aliyekuwa akiishi sehemu hiyo kutoweka na mwanao msichana wa miaka 14 ambaye ni mwanafunzi wa darasa la nane katika shule ya msingi ya Emusonga.

Familia hiyo kupitia kwa babake mwanafunzi huyo Michael Shikanda Mukabana inasema kuwa mshukiwa huyo ambaye anatoka ebeo bunge la Khwisero alikuwa amegodisha nyumba kwenye boma lao kabla ya kutoweka na mwanafunzi huyo  aliyekuwa amekamilisha darasa la saba akingojea kujiunga na darasa la nane tarehe nane mwezi wa sita mwaka huu.

Kulingana na familia hiyo juhudi zao za kuwasaka wawili hao ili mwanafunzi huyo aendelee na masomo yake zimeambulia patupu na kutaka yeyote aliye na habari walipo kuwapigia simu au kuripoti kwenye kituo cha polisi kilichoko karibu.

By Lindah Adhiambo

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE