Biwi la zimanzi limetanda katika kijiji cha Iseka kaunti ndogo ya Nambale Kaunti ya Busia baada ya mwanamume mmoja kupatikana akiwa ameaga dunia kwenye shimo la Choo la mkaazi mmoja kijijini humo.

Kwa mjibu wa familia yake, marehemu Lazaros Wandera mwenye umri wa miaka 31 alikuwa ameenda kunywa pombe haramu ya chang’aa katika boma hilo, na huenda alitumbukia kwenye shimo hilo kutokana na ulevi alipokuwa akirejea nyumbani kwake.

Wenyeji wa eneo hilo wamelalamikia kukithiri kwa unywaji wa pombe haramu ya changaa miongoni mwa vijana wa umri mdogo.

Pia wamelalamikia hatua ya wananchi kuchimba mashimo na kuyaacha wazi ambayo yanahatarisha maisha ya wakazi.

By Hillary Karungani

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE