Biwi la simanzi limetanda katika kijiji cha Tande eneo bunge la Malava baada ya mwanamme mwenye umri wa miaka 31 kwa jina Emmanuel Nasong’o kupatikana akiwa amejitia kitanzi ndani ya nyumba yake.

Kulingana na mmoja wa majirani za marehemu ni kuwa alikuwa katika harakati za kuweka ua kwenye shamba lake la mboga lililoko nyuma ya nyumba ya mwendazake kabla ya kukutana na mwili wake ukiwa unaning’inia ndani ya nyumba hiyo.   

Akidhibitisha kisa hiki naibu chifu wa eneo hilo John Chisembe ambaye ametumia fursa hiyo kuwarai  wakaazi wa eneo kutafuta ushauri nasaha wanapokumbana na matatizo badala ya kujitoa uhai.

Kwa sasa mwili wa mwendazake unahifadhiwa katika chumba cha wafu kwenye hospitali ya rufaa ya Kakamega ambako unatarajiwa kufanyiwa upasuaji ili kubaini chanzo cha kifo chake.

By Imelda Lihavi

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE