Jamaa mmoja anazuiliwa katika kituo cha polisi kwa kupiga mkewe hadi kifo baada ya kumpata katika kibanda cha chang’aa akiwa mlevi chakari.

Kevin Onyango mwenye umri wa miaka 34, anaripotiwa kumshambulia mkewe Emmaculate Mayavi wa umri wa miaka 42, kwa kumpiga teke na ngumi baada ya kumpata kwa  baa moja inayouza chang’aa iliyo katika kijiji cha jera eneo la ugenya, kaunti ya siaya.

Kulingana na DCI, Onyango alirejea nyumbani kwake mida ya jioni siku ya Jumamosi na kumkosa mkewe na hapo akapiga hatua ya kumtafuta.

Baada ya kumtafuta kwa alipata mkewe akiwa amepoteza fahamu kutokana na kubugia kiasi kikubwa cha chang’aa. Na kwa hasira Onyango akampiga mkewe vibaya kisha akambeba kwa troli hadi nyumbani kwao.

Inaripotiwa kuwa baadae usiku wa Jumamosi bi.Mayavi aliaga dunia kufuatia matatizo ya mwili ambayo alipata kutokana na kichapo  alichopokea

Polisi kutoka kituo cha Siaya walimkamata mshukiwa na anatarajiwa mahakamani kujibu mashtaka ya mauaji. Mwili wa marehemu ulipelekwa katika chumba cha kuhifadhi wafu cha hospitali ya siaya kwa uchunguzi zaidi

By Imelda Lihavi

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE