Mwanamme mwenye umri wa miaka 23 kwa majina Dickson Mike amepatikana akiwa amafariki kwa njia tatanishi kwenye chumba kimoja cha burudani katika soko la Kambi Mwanza eneo bunge la Malava.

Kulingana na naibu chifu wa kata ndogo ya Kakunga Jackson Ambulwa ameelezea kituo hiki kuwa mwili mwendazake ulipatikana baada ya mpita njia kuchungulia ndani ya chumba hicho huku duru zikiarifu kuwa  huenda marehemu aliuawa na watu wasiyojulikana.

“ kuna mtu alikua anapita akachungulia kwa dirisha akaona mtu ni kama amekufia ndani kwa sababu pazia haikua kwa dirisha. Nilipewa ripoti nikaita askari tukabomoa mlango, na kulikua na damu kwa floor nadhani hiyo ndo ilikua imemuafect lakini pia alikua ni kama alijihung kwasababu alikua na nguo amefunga kwa  shingo.” Alisema naibu chifu.

Ambulwa aidha amehoji kuwa ameshangazwa na  namna mwendazake alivyofariki akihoji kuwa huenda kifo chake kilitokana na mzozo wa kimapenzi au marehemu alitofautiana na wanzake kabla ya kuawa.      

cha kushangaza ni kwamba huyo kijana hakua na long’i alikua na t-shirt pekeyake. Ni kama aata kama hakua na mpenzi wake labda ni watu tu waliomfanyia hivyo. Na akaamua kujifungia ndani.” Alielezea naibu chifu

Hata hivyo mtawala huyo amewataka wamiliki wa maeneo yote  ya burudani kuwa waaangalifu na wateja wao kama njia mojawapo ya kuzuia visa sawia.

Tayari  maafisa wa usalama wameanzisha uchunguzi kamili ili kubaini chanzo cha kifo hicho.

Story by Javan Sajida

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE