Mgombezi wa kiti cha eneo bunge la Matungu kupitia chama cha UDA kwenye uchaguzi mdogo Alex ,Lanya amepigwa jeki baada ya Eugene Murunga mwanawe aliyekuwa mbunge wa eneo hilo marehemu Justus Murunga aliyekuwa ameidhinishwa na IEBC kutangaza kumuunga mkono ana Paul Posho.

Eugene akiwa na wagombezi wengine wapatao watano ambao walitangaza azma yakuwania kiti hicho japo hawakuidhinishwa na IEBC wameamua kwa kauli moja kumuunga mkono Lanya kwenye safari yake ya kutafuta kiti hicho.

Huku mbunge wa Mumias Mashariki Benjamin Washiali akimsuta mbunge wa Suna East Junet Mohammed kuwa wakazi wa Matungu wakimchagua David Were wa chama cha ODM atawekwa kwenye kamati ya kilimo ili kumwezesha kufufua kiwanda cha Mumias.

Naye aliyekuwa seneta wa Kakamega DKT. Boni Khalwale, akipuuzilia mbali madai kuwa huenda chama cha ODM kikisaidiwa na serikali kuiba kura Matungu.

Paul Posho alimtaka gavana wa Kakamega Wycliffe Oparanya kusitisha vitisho kwa wafanyikazi wa kaunti  wanaotoka Matungu kuwa huenda wakapoteza kazi iwapo wataunga mkono ,Lanya.

Alex Lanya alitumia fursa hiyo kuwataka wakazi kumuunga mkono ili kuendeleza miradi zilizoachwa na Murunga.

Story by Kefa Linda

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE