Hofu imetanda katika mtaa wa Eshiakhulo eneobunge la Mumias Mashariki baada ya mwili wa mwanamme mmoja kupatikana ukiwa na kamba shingoni Kwenye uwanja wa shule ya upili ya Eshiakhulo
Mwili huo ulopatikana Leo asubuhi ulikuwa na kamba shingoni dhibitisho kuwa mwendazake alijinyonga
Chifu wa kata ndogo ya Khaimba Mary Njaya amesema kuwa mwili huo ulikuwa na majeraha shingoni
Chifu huyo amehusisha kifo hicho na mizozo ya kifamilia akiwataka wakaazi kutafuta mbinu mwafaka ya kusuluhisha migogoro hiyo
Mwili wa mwendazake umeenda kuhifadhiwa kwenye makafani ya hospitali ya kimishenari ya St Mary’s Mumias
Story by James Nadwa