Huenda mzozo kati ya bunge la kaunti ya Bungoma na gavana wa kaunti hii Wycliffe Wangamati ukaendelea kutokota hata zaidi huku baadhi ya wawakilishi wadi wakishikilia msimamo kuwa lazima ugavi wa mipaka ya vijiji ufanyiwe marekebisho kabla kuwaajiri wasimazi wa vijiji hivyo (village administrators).

Akihutubu kwenye hafla ya mazishi katika kijiji cha Tulienge eneo bunge la Sirisia naibu kiongozi wa wachache katika bunge la kaunti ya Bungoma Tonny  Barasa, amesema atazidi kupinga uajiri wa wasimamaizi wa vijiji hadi swala la mipaka litakapoangaziwa kwa kina.

Barasa ambaye pia ni mwakilishi wadi ya Lwandanyi katika bunge la kaunti ya Bungoma ametoa wito kwa viongozi wa siasa kusitisha siasa za matusi na badala yake kuwajibikia majukumu yao kwa wananchi.

By Hillary Karungani

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE