Huku mzozo ukizidi kutokota katika chama cha ANC tawi la Malava mkurugenzi mkuu wa chama  hicho kaunti ya Kakamaga Isaac Otiende amesema kuwa chama hicho kimeanzisha mikakati ya kuona kuwa suluhu mwafaka kuhusiana na kuwepo kwa afisi mbili za anc eneo hilo linapatikana.

Akizungumza baada ya kuzuru afisi ya chama hicho mjini Malava, Otiende amehoji kuwa kuwepo kwa mzozo huo ni ishara tosha kuwa chama hicho kinazidi kupata umaarufu huku akiahidi wanachama wa ANC kuwa suluhu mwafaka litakuwa limeafikiwa kabla ya uchguzi mkuu ujao wa mwaka wa 2022.

Aidha Otiende amewarai viongiozi wengine kutoka eneo la Magharibi kujiunga na chama hicho katika juhudi za kuona kuwa kinara wa chama cha ANC Musalia Mudavadi anatwaa uongozi wa taifa hili.

Kwa upanede wake mwenyekiti wa chama hicho tawi la Malava Francis Murambi amesema kuwa tayari usajili wa wanachama wa kujiunga na chama hicho unaendelea katika eneo zima la Malava.

By Richard Milimu

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE