Maulid Wanjala wa eneo la Lukume, lokesheni ya Lukume wadi ya West Kabras, Kakamega Kaskazini ameichukua jukumu kama naibu Chifu mpya wa eneo hilo, kuwahasirisha vijana na kuwaonya juu ya matumizi ya pombe na kucheza kamare.

ingawa vijana wengi hapo awali walipendelea kutengeneza pombe, kuitumia na kucheza kamare, ameanza kuona mabailiko. Haya yalifanyika tu baada yao kutembea vijijini na kuwahamasisha vijana kuhusu athari yao.

Akiwa pamoja na chifu wa eneo hilo Bwana Maliki Shanguia, Anawasihi vijana kuacha vitendo viovu vinavyo weka maisha, afya na akili zao hatarini na badala yake kujiunga na biashara ili wajijenge.

Hapo awali, vijana hawa walipomwona walitoroka, lakini sasa anasema wamebadilika na kumtafuta ili awaelemishe.

 vijana hawa wameapa kubadili mienendo lakini wanaiomba serikali iwasaidie.Kwa upande wake amewaelezea kuhusu YouthFund,uwezo Fund na Women Enterprise. Ambazo ni mikopo inazoweza kuwasaidia lakini yafaa wakuje kwa vikundi.

Kadhalika hamna hoja kwa kazi yake ni nzuri ila lazima uzingatie sharia na uitekeleze aidha wananchi wako tayari kujitolea na kudadili maisha yao kulingana na hali. 

Story by Laura Mmosi

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE