Mwakilishi wa Wadi ya Lwandanyi katika eneo bunge la Sirisia Kaunti ya Bungoma Tonny Baraza, ameyapuzilia mbali madai kuwa ametimuliwa katika wadhifa wa Naibu Kiongozi wa wachache katika bunge la Kaunti ya Bungoma.

Kwenye taarifa kwa wanahabari, Baraza amesema hadi sasa hajapokea taarifa yoyote kutoka kwa spika wa bunge hilo kuhusu mabadiliko kwenye uongozi wa Jubilee katika bunge la Bungoma.

Ameshikilia kuwa bado anahudumu katika wadhifa huo, na kwamba uvumi huo unaenezwa na wapinzani wake kisiasa kufuatia msimamo wake kupinga utaratibu unaotumiwa na gavana wa Kaunti ya Bungoma Wycliffe Wangamati kwenye mchakato wa kuajiri wasimamizi wa vijiji.

By Hillary Karungani

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE