LUBAO FREQUENCY MODULATION LIMITED

Uniting Communities
  1. Listen to Lubao FM Live 102.2 FM

Live now:

Up next:

Ng’ombe kuwawa na nyuki katika eneo la Butsotso Mashariki kaunti ya Kakamega

Mama mmoja mjane na wajuku wake kutoka kijiji cha Shitirira wadi ya Butsotso mashariki eneo bunge la Lurambi kaunti ya Kakamega walisurika kifo huku ng”ombe wake wa kipekee akifariki baada ya kuvamiwa na nyuki katika boma lake.

Mary Atemba ambaye ni mwasiriwa anasema alikuwa ndani ya nyumba yake kabla ya kusikia wajukuu wake wakipiga mayowe na kuingia Kwa nyumba japo alipotoka nje kutazama kilichokuwa kikijiri,alimpata ng”ombe wake akiwa amevamiwa na nyuki hao na alipojaribu kumuokoa ng”ombe huyo ndiposa nyuki hao wakamgeuka.

Anasema kuwa alitoroka na majeraha japo nyuki hao walimuua ng”ombe huyo

“Mimi nimeponea chupuchupu na huyu mjukuu wangu kwa sababu nyuki ingetuuwa. nyuki hizi zimekuja tu zikavamia ng’ombe na pia zikatuvamia na sasa ng’0mbe yangu imekufa na ni ng’ombe yangu ya kipekee. ndo kitu nilikua nacho cha kipekee. “ alisema mama

Kulingana na Mwasiriwa anasema kuwa nyuki hao wanaishi kwenye nyumba ya jirani na kutoa wito Kwa idara husika kuingilia kati kuwafurusha nyuki hao kuzuia maafa zaidi.

By Kefa Linda

Charles Oduor

Read Previous

CHANJO YA COVID_19 YAIBUA MITAZAMO TOFAUTI MIONGONI MWA VIONGOZI WA KIDINI.

Read Next

Neymar kuingia Makubaliano ya awali ya kuichezea St Germain mpaka mwaka 2026

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *