Ipo haja kwa wazazi kuwa karibu na wanao kwa kuhakikisha wana nidhamu  na maadili mema ili wasije wakakatisha ndoto yao ya maisha kwa kujihusisha kwenye visa potovu.

Akizungumza huko Shibuli naibu wa chifu wa eneo hilo Samwel Shilabile amesema kuwa watoto wamepotoka kinidhamu baada ya kukaa nyumbani kwa muda mrefu akitaja kisa kimoja ambapo wanafunzi wa shule moja eneo la Shisiru katika eneo bunge la Lurambi walipatikana na bidhaa za wizi ambazo ziliaminika kuibwa katika duka la mfanyibiashara moja kwenye soko la Shisiru.

Naibu huyo wa chifu na mwenzake wa Shiyunzu Butsotso ya kati kwa pamoja wamesisitiza umuhimu wa watoto wote ambao wanafaa kuwa shuleni kusalia shuleni ili wasije wakajiunga na  vikundi ambavyo vimepotoka kinidhamu na kujipata pabaya kwa mkono wa kisheria.

Swala hili la watoto kupotoka kinidhamu  limeonekana wazi baada ya watoto kurejea shuleni siku kumi zilizopita na kunastahili wadau wote kuungana na kuwapa ushauri nasaha wanafunzi bila kuachia tu walimu kama alivyosema mwalimu mkuu wa shule ya Eshiamboko iliyoko eneo bunge hilo Josephat Chimwani…

Story by Richard Milimu

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE