Kampuni ya kusambaza maji ya NZOWASCO inazidi kulaumiwa pakubwa kufwatia ukosefu wa maji na kudaiwa kutoa huduma duni kwenye wadi ya Chesikaki eneobunge la Mlima Elgon.

Akihutubu kwenye hafla ya mazishi eneo la Chesikaki mwakilishi wadi wa eneo hilo Ben Kipkut  anasema masaibu ya ukosefu wa maji katika wadi ya Chesikaki yametokana na utepetevu wa kampuni ya NZOWASCO akidokeza kuwa  hataruhusu kampuni hiyo kutoa huduma kwa wakaazi.

Wakati uo huo Kipkut amedokeza kuwa hivi karibuni serikali ya kaunti ya Bungoma itaanza kukarabati barabara ya kutoka shule ya upili ya marafiki ya kimabole kuelekea Mulukhu ambapo tayari shilingi milioni mbili nukta tano zimetengwa kwa shughuli hiyo.

Amewasihi wananchi kuzingatia masharti ya wizara ya afya katika juhudi za kupambana na maambukizi ya virusi vya corona.

By Richard Milimu

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE