Kufwatia ongezeko la visa vya kujitoa uhai eneobunge la Mumias Mashariki vyongozi eneo hilo sasa wanawataka wakaazi kutafuta mbinu mwafaka za kusuluhisha mizozo

Akizungumza kwenye hafla moja ya mazishi mtaa wa Makunga B eneobunge la Mumias Mashariki ambapo mwendazake aliripotiwa kujitoa uhai mwanasiasa Peter Salasya amesema kuwa wingi wa visa hivyo hutokana na msongo wa mawazo

 Amewataka wakaazi kutafuta usaidizi badala ya kuchukua hatua ambazo huwenda zikawagharimu maisha yao

Vile vile alielezakua kuwa iwapo atafaulu kuingia katika afisi za CDF eneobunge la Mumias Mashariki baada ya uchaguzi mkuu atabuni vitengo vya kukabili na kutatua tatizo hilo

Salasya hata hivyo amewaonya wakaazi dhidi ya kufuja chakula haswa wakti huu wa mavuno

By James Nadwa

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE