Swala la ufufuzi wa kiwanda cha sukari cha Mumias linaonekana kuchukua mkondo mpya huku viongozi wa kutoka kaunti ya Kakamega wakinyosheana kidole cha lawama kwa kuwa kizingiti kwa mchakato mzima wa kuhakikisha kuwanda hicho kinarejelea shughuli zake za kawaida

Seneta wa kaunti Kakamega Cleophas Wakhungu Malala amemshutumu gavana wa kaunti hiyo Wycliffe Oparanya kwa kushindwa kuweka wazi masaibu yanayokumba kiwanda hicho na badala yake anashirikiana na mwekezaji mwenye kukosa nia ya kufufua kiwanda hicho kwa maslahi ya kibinafsi

Malala anadai ni lazima kuwepo na utaratibu wa kisheria kwenye swala na mwekezaji mwenye nia na uwezo wa kufufua kampuni hiyo huku akikashifu hatua ya afisi ya gavana Oparanya kwa kuficha baadhi ya barua ambazo wakezaji wenye nia njema hutuma kwake

Nao wakulima wakiongea katika eneo la Makunga Mumias Mashariki baada ya kukutana na seneta huyo, wanamewataka wanasiasa kusitisha siasa zao kuhusu kiwanda na kushikilia kuwa wao wakotayari kukumbatia yule mwekezaji yeyote ambaye atawakwamua kutoka kwa masaibu ya kiwanda hicho

By  Linda Adhiambo

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE