Exif_JPEG_420

Waumini wa kanisa la pentacostal makao church katika kaunti ya bungoma sasa wana kila la kutabasamu baada ya askofu mkuu wa kanisa hilo lenye makao yake makuu mjini malava kakamega, Bishop Timothy Juma kufungua rasmi na kukabidhi cheti cha kanisa hilo na bendera.

Akiongea na kituo hiki baada ya ibaada Askofu Mkuu Timothy Juma amewataka viongozi wa kanisa hilo mpya la “saawa pentacostal makao church” linalopatikana katika kijiji cha saawa, wadi ya maanga, eneo bunge la Webuye Magharibi kaunti ya Bungoma, kuwa na ushirikiano mwema ili kufikia wengi kwa neno la mungu.

Amewataka kuwa na mfano mwema wanapoendeleza huduma ya mungu ili kuwaleta wengi kwa kristo.

Naye kwa upande wake kiongozi wa akina mama kwenye ngazi ya kitaifa (mama kenya) Annah Mula, amewahimiza akina mama wa kanisa hilo kukaza mwendo katika maombi na kuona kwamba neno la mungu linasambaa kote nchini huku mchungaji wa assembly hiyo ya saawa vincent atomia akishukuru kwa kukabidhiwa cheti hicho.

Wycliffe Sajida

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE