Oparesheni zidi ya pombe haramu ya chang’aa imefutiliwa katika wadi ya Isukha Kusini eneo bunge la Shinyalu kaunti ya Kakamega baada ya wahudumu wa serikali ya kitaifa na kaunti wakiwa   na  manaibu chifu,  chifu, community administrator, ward administrator pamoja na wakaazi wa maeneo hayo kuja pamoja katika mkutano uliyoitishwa na Wycliffe Lijina ambaye ni community administrator wa Museno uliyofanyika katika kanisa katoliki Museno na kupiga marufuku pombe haramu ya chang’aa.

Mkutano huo ambao ulihudhuriwa na mwelekezi kuhusiana na vileo (county director alcoholic drinks) katika kaunti ya Kakamega Benson Ochomo, ambaye anawahimiza wakaazi wa Isukha Kusini kujiepusha na vileo vya pombe ya chang’aa ili kupisha maendeleo katika jamii.

Benson anashauri kwamba utumiaji wa pombe ni chanzo cha kuhatarisha na kufupisha na vilevile pombe haramu husababisha magonjwa.

Hata hivyo viongozi hao kwa pamoja na wakaazi wanatoa pendekezo kwa serikali ya kitaifa na mahakama kuzidisha faini hadi shilingi elfu hamsini 50k badala ya shilingi mia tano kwa yule ambaye atapatikana akiuza pombe ya chang’aa.

Vilevile kwenye mkutano huo wanaiomba idara ya polisi kwa wale wenye tabia za kuitisha shilingi elfu tano kutoka kwa mpika pombe kuwacha tabia hiyo ili kusaidia kuangamiza pombe haramu.

Wycliffe Lijina ambaye ni community administrator wa Museno anatoa agizo kwa wakaazi wake kushugulikia maendeleo na nidhamu kwa wakubwa na wadogo sawia na kujijali kiafya.

Ni mkutano uliyong’oa nanga saa nne za asubuhi na kukamilika mwendo wa saa nane mchana saa za afrika mashariki.

Ulihudhuriwa na jumla ya watu hamsini na wahudumu wa serikali kumi na wanne.

Mkutano mwingine utakaofanyika unapania kushirikisha viongozi wa kisiasa na wa serikali.

By Wycliffe Sajida

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE