Rais Uhuru Kenyatta  amekosolewa vikali kufwatia uteuzi wa majaji wa mahakama hivi majuzi huku viongozi wa kisiasa  kutoka jamii ya Mulembe wakidai eneo la Magharibi mwa nchi liliachwa nje kwenye uteuzi huo wa majaji.

Akihutubu eneo la Musese kwenye hafla ya kuzindua ugavi wa hundi za basari kwa wanafunzi elfu tano warevu wa shule za upili na vyuo vikuu  kutoka jamii maskini eneobunge la Kabuchai, mbunge wa eneo hilo Majimbo Kalasinga amehoji kuwa uteuzi huo wa majaji haukuhusisha sura kamili ya kitaifa hasa eneo la Magharibi likiachwa nje.

 Naye mbunge wa kwanza kaunti ya Trasnzoia Ferdinad Wanyonyi  amedai licha ya jamii ya mulembe kuwa ya pili kwa idadi ya wakaazi hakuna jaji yeyote aliyeteuliwa kutoka eneo hili akidokeza kuwa watajadili swala hilo  kabla hatua mwafaka kuchukuliwa.

Kadhalika Majimbo amemtaka rais Uhuru Kenyatta kuhakikisha kuna usawa wakati wa kuzindua miradi ya maendeleo katika sehemu mbalimbali humu nchini.

By Hillary Karungani

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE