Naibu rais William Ruto amewashambulia viongozi wa National Super Alliance, na kuwaambia wampe rais Uhuru Kenyatta muda wa kufanya kazi kwa wakenya.

Akiongea huko Huruma ambapo alihudhuria ibada ya kanisa katika African Holy Ghost Christian Church Jumapili, Ruto alisema kuwa rais alichaguliwa kuhudumia wakenya zaidi ya milioni 45 na wala si watu wachache tu.

Kigogo huyo amewakosoa  viongozi wa NASA  kwa kubadilisha mwelekeo wa mkuu wa nchi kuwaunganisha kwa sababu hawawezi kukubaliana kati yao, baada ya juhudi za kubadilisha katiba kutupiliwa mbali.

Korti ya rufaa bado haijatoa uamuzi juu ya rufaa ya mchakato wa BBI ambayo ilisikilizwa na benchi saba la majaji.

By Sajida Javan

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE