Serikali ya kaunti ya Bungoma kupitia wizara ya afya imetenga shilingi milioni tisa nukta nane zitakazofanikisha upanuzi wa hospitali ya kaunti ndogo ya Cheptais eneobunge la Mlima Elgon ili kuboresha huduma za afya.

Akihutubu kwenye hafla ya mazishi eneo la Cheptais mwakilishi wadi ya Cheptais bi Jane Chebet amehoji kuwa fedha hizo zitasaidia kuimarisha miundo msingi hospitalini humo huku akidokeza kuwa zahanati ya Chebwek Nalondo na kang’anga  zitaboresha huduma za afya eneo hilo pindi ujenzi utakapomalika.

Aidha bi Chebet ameshikilia msimamo wa kutaka eneobunge la Mlima Elgon kugawanywa mara mbili kupitia mchakato wa BBI.

Ametangaza kuwania kiti cha ubunge eneo la Mlima Elgon kwenye uchaguzi mkuu ujao akisema katiba inamruhusu kila mkenya kuwania kiti chochote cha kisiasa.

story by Imelda Lihavi

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE