Serikali imetakiwa kuchunguza na kuwakamata wale wanaoiba na kuharibu misitu ya serikali ya Kakamega na Malava wakati huu ambapo taifa linang’ang’ana kuhakikisha linatimiza agizo la asilimia kumi ya miti nchini.

 Ni kauli ya mwenyekiti wa shirika la kutetea masilahi ya wakulima nchini la Kenaff tawi la kaunti ya Kakamega  Habakuk Khamala baada ya kuzindua upanzi wa miti katika shule ya msingi ya Ebuchinga kata ndogo ya shibuli eneo bunge la Lurambi.

 Mwenyekiti huyo pamoja na mshirikishi wa shirika hilo kanda ya Magharibi mwa Kenya Pius Akhonya wamesema kuwa shirika hilo linaungana na Taifa la Kenya kuafiki lingo la kupanda miti bilioni 2 kufikia mwaka 2022 na kuhimiza wakulima kukumbatia wito huo na kupanda miti katika makaazi yao.

Naye kaimu chifu wa eneo hilo Samuel Shilabile akapongeza juhudi za serikali kuu na ile ya kaunti ya Kakamega kuweka ua katika msitu wa Kakamega akisema kuwa hilo litasaidia kulinda msitu huo kutokana na wezi na unyakuzi.


By Boaz Shitemi

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE