Shambulio la kuvizia dhidi ya msafara wa maafisa wa usalama nchini Burkina Faso uliokuwa ukisafirisha malori ya mafuta kutoka kwenye mgodi wa machimbo ya dhahabu, karibu na mpaka wa Niger limewauwa maafisa wa usalama sita, maafisa wanasema.

Watu saba wamejeruhiwa baada ya kile ambacho serikali ya jimbo Mashariki mwa Burkina Faso ilisema lilikuwa ni shambulio la jihadi. Miaka miwili iliyopita watu 39 waliuawa wakati msafara wa magari uliokuwa ukitoka eneo hilo hilo kushambuliwa.

Tukio hilo lilisababisha kufungwa kwa shughuli za uzalishaji kwa takriban mwaka mmoja.

Tangu mwaka 2015 mashambulio ya makundi yenye uhusiano na islamic state na al-qaeda wamewauwa zaidi ya watu 1,500 na kuwalazimisha zaidi ya milioni moja wengine kuyahama makazi yao.

By Wycliffe Andabwa

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE