Waumini wa dini ya kiislamu kutoka Cheptais eneobunge la Mlima Elgon wamejumuika katika sherehe za Iddul-Fitr kwenye msikiti wa Jamia huku wito ukitolewa kwa wananchi wote kuzingatia masharti ya wizara ya afya ili kukabili msambao wa virusi vya corona.

Akihutubu baada ya sherehe za Iddul-Fitr mwakilishi wadi ya Cheptais bi Jane Chebet amesema virusi vya corona vimesababisha waumini wa dini ya kiislamu kutoandaa sherehe hizo na wataka wananchi kufwata mwongozo wa serikali ili kupambana na homa ya corona.

Aidha bi Chebet amedokeza kuwa licha ya kuwepo changamoto hiyo amejitolea kutoa msaada wa chakula kwa waumini hao ili kusherehekea siku hii.

Anasema atazidi kushirikiana na waumini hao ili kufanikisha elimu ya wanao huku karani wa msikiti huo Abdul Kareem akipongeza juhudi za mwakilishi wadi huyo kuunganisha jamii ya kiislamu.

By Hillary Karungani

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE