Shule zimerekodi idadi kubwa ya wanafunzi leo hii ikiwa ni siku ya kwanza kwa wanafunzi kurudi shuleni tangu mwezi mechi mwaka jana baada ya amri ya rais uhuru kenyatta kuwa shule zote nchini kufungwa kutokana na janga la virusi vya corona licha ya kuwa na hofu miongoni mwa wazazi  pamoja na wanafunzi.

Agrrey shichere ambaye ni mwalimu mkuu katika shule ya upili ya kakamega township kwenye wadi ya shirere eneo bunge la ikolomani kaunti ya kakamega amesema kuridhishwa na idadi hiyo ya wanafunzi shuleni hata baada ya shule hiyo kuwa na idadi kubwa ya wanafunzi wa kike ikilinganishwa na ile ya wanaume.

Wakati uo huo shichere amewataka wazazi kushughulikia swala la kulipa karo ya wanao kwa upesi ili wanafunzi wapate kuwa na mazingira mema ya kusoma baada ya kukosa masomo kwa muda mrefu wakiwa nyumbani.

Hali sawia na hiyo imeshuhudiwa katika shule jirani ya msingi ya kakamega township huku zaidi ya wanafunzi mia nne kati ya wanafunzi mia sita wakifungua shule leo.

Akizungumza na kituo hiki fresher ayaya ambaye ni naibu mwalimu mkuu katika shule hiyo amefichua kuwa shule hiyo inapitia changamoto ya ukosefu wa walimu ikizingatia kuwa walimu wawili katika shule hiyo wana umri wa zaidi ya miaka 58 jambo ambalo litapunguza idadi ya walimu shuleni humo.

Story by  richard milimu

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE