Huku shamrashamra za matokeo zikiendelea kushuhudiwa kote nchini shule ya msingi ya Mtakatifu Agostino Lubao ina kila sababu ya kusherehekea baada ya mwanafunzi wa kwanza kwenye shule hiyo kujizolea alama 404 kwenye mtihani wa kitaifa wa KCPE ambao matokeo yake yalitangazwa rasmi na waziri wa elimu nchini Profesa George Magoha

Cynthia vitakwa amewaongoza wenzake kwenye shule ya msingi ya Lubao kwa kuzoa jumla ya alama 404 

Akizungumza na  Idhaa hii, Cynthia ameelezea furaha yake ya kupita mtihani huo na kuwapa motisha wenzake ambao wanahisi hawajafanya vyema kwenye mtihani huo

Cynthia amesema kuwa atajiunga na shule yake ya ndoto ya muda mrefu ikiwa ni shule ya wasichana ya Pangani

Kwa upande wake mlezi anayekaa na Cynthia ambaye ni shangaziye Joyce Kageha ameelezea furaha yake baada ya matokeo hayo  na kupongeza juhudi za Cynthia kutia fora kwenye masomo yake huku akisema kama familia wapo tayari kumruhusu kujiunga na shule yake ya ndoto ya muda mrefu ya wasichana ya pangani 

Kwa upande wake mwalimu mkuu wa shule hiyo Kennedy Indeche amesema kuwa kwa jumla watahiniwa themanini na nane walikalia mtihani huo kwenye shule hiyo lakini kufikia sasa wamepata matokeo ya wanafunzi 19 ambao wote wamezoa jumla ya alama 300 na zaidi wakisubiri kupata matokeo zaidi hapo kesho

By Sajida Javan

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE