Kocha wa timu ya mpira wa kandanda ya shule ya upili ya wasichana ya Mwira kutoka eneo bunge la Matungu inayoshiriki kwenye ligi ya kitaifa divisheni ya kwanza ya Nyuki Starlets Edgar Akhonya ameshukuru kusajiliwa kwa wachezaji wawili wa timu hiyo akiwemo nahodha wake Esta Amakobe na mshambulizi Phenanic Wamalwa kujiunga na kikosi cha taifa huku akimtaka waziri wa michezo Amina Mohammed kuruhusu kurejelewa kwa michezo kuwawezesha wachezaji kujiandaa kuwakilisha nchi kwenye mechi za kimataifa.

Akizungumza akiwa eneo bunge la Matungu , kocha Akhonya  amesema kuwa wawili hao wamesajiliwa kujiunga na kikosi cha taifa na kwa sasa wanajiandaa kusafiri hadi jijini Nairobi kujiunga na timu hiyo huku akisema kuwa kusitishwa kwa michezo nchini kuthibiti msambao wa virusi vya corona kumeathiri wachezaji wengi.

Kulingana na Akhonya ameitaka serikali kupeana chanjo kwa wachezaji wote  na kurusu kurejelewa kwa michezo nchini kwani timu yake ilikuwa ya tatu kwenye jedwali ya ligi hiyo ya kitaifa divisheni ya kwanza kabla ya kusitishwa kwa michezo.

By Richard Milimu

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE