Mbunge wa Shinyalu Justus Kizito Mugali ametakiwa kuweka wazi jinsi mgao wa pesa za basari zinavyopeanwa kwa wanafunzi kwenye eneo bunge hilo 

Ni usemi wake aliyekuwa mbunge wa eneo hilo Sylverse Anami Lisamula akizungumza kwenye ibaada ya maombi na mazishi ya mzee Joab Mwinami Lukhavi sehemu za Murhanda eneo bunge la Shinyalu kaunti ya Kakamega 

Akirejelea kwenye uongozi wake Lisamula amesema ni haki ya kila mwanafunzi kupata mgao huo kwa njia ya uwazi 

Wakati uo huo Lisamula amempigia debe kinara wa chama cha ANC Wycliffe Musalia Mudavadi kutwaa uongozi wa taifa hili na kuwataka wakaazi wa magharibi mwa Kenya kumuunga mkono Mudavadi kwenye safari hiyo

Lisamula amemkosoa gavana wa kaunti ya Kakamega Wycliffe Oparanya kwa kutokamilisha miradi ya maendeleo haswa aliyoanzisha kwenye eneo bunge la Shinyalu ikiwemo ujenzi wa barabara ya kuelekea Chepsonoi kupitia Shinyalu, ujenzi wa hospitali ya Shamakhuvu na kiwanda cha majani chai cha Madala akiwataka viongozi waliochaguliwa kufwatilia miradi hiyo kuona kuwa gavana Oparanya anaikamilisha kabla ya muhula wake kutamatika mwaka ujao

Hata hivyo kulizuka majibizano makali ya kisiasa baada ya mwakilishi wadi wa Shirere David Ikunza kusifia utendakazi bora wa mwakilishi wadi ya Murhanda Elphas Shilosio, huku Patrick Chungani akimtaka mwakilishi huyo kutoingilia siasa wala maendeleo ya sehemu za Murhanda kwa kusema hamna cha wakaazi wa sehemu hizo wanajivunia kwa uongozi wa Shilosio kufikia sasa akieleza matumaini ya kutwaa kiti hicho

Hata hivyo Shilosio ameahidi kushindana naye wazi akisema Chungani hana msimamo wa kisiasa kwani kila baada ya uchaguzi amekuwa akisimama viti ngazi tofauti tofauti 

Hata hivyo mwakilishi huyo wa Murhanda amelalamikia mapendeleo ya maendeleo kutoka kwa mbunge wa sehemu hiyo Justus Kizito ambaye ametenga wadi hiyo kimaendeleo

Shilisio amesema kizito amedinda kuleta maendeleo kwenye wadi hiyo kwa kisingizio kuwa wakaazi wa wadi hiyo hawakumpigia kura kwenye uchaguzi mkuu uliopita na kulalamikia pia ujenzi wa shule na mgao wa basari unavyoendeshwa kutoka nyumbani kwake mbunge huyo.

By Javan Sajida

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE