Wakazi wa kaunti ya kakamega wmeendelea kukashifu agizo la serikali ya kaunti la kuazuia wakazi wanaoishi mijini kuwazika wapendwa wao kwenye maboma ya miji

Ni utata uliotokea baada ya kifo cha aliyekuwa afisa mkuu katika wizara ya kilimo daktari Kelly Nelima ambaye mazishi yake yaliyokuwa yameparatibiwa kufanyika jumamois iliyopita katika boma lake mtaa wa Kefnco yalisimamishwa na agizo la serikali ya kaunti kwa madai kuwa boma lake liko mjini 

 Inasemekana ufadhili wa benki kuu umetoa masharti ya kuweza kutekelezwa baada katika juhudi za kuufanya mji wa Kakamega kuwa mji mkuu na baadhi ya wakazi akiwemo kiongozi wa vijana katika wadi ya Sheywe Gilbert Alushiula wamekuwa na maoni tofauti

“Tukiangalia katika wadi mingi tunaona maisha ya wanannchi yote ni hapo na pia wana nambari za usajili wa shamba hapo. Maneno ya kusema watu wasizikwe katika wadi ambazo ziko karibu na mji na kukatalia utamaduni si vyema maana mazishi kwa waluhya ni kama utamaduni. Ni vizuri gavana akae na wanannchi na wawe na mahojianao ya moja kwa moja.”

Alushiula ameungana na wakazi kuwataka wawakilishi wadi kuwajibikia jukumu lao na kuona kwamba wananchi hawahangaishwi


Story by Boaz Shitemi

sadmin

By sadmin

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE