Mbunge wa Lurambi Askofu Titus Khamala anawataka viongozi wa kidini kuwazuia wanasiasa kuhutubia hafla za matanga kuepuka vurumai inayoshuhudiwa kwa sasa hasa katika eneo la Matungu ambalo linajitayarisha kwa uchaguzi mdogo

 Akihutubu kwenye mazishi ya shangazi wake Beatrice Khayeli kata ndogo ya Shibuli Butsotso ya kati Askofu Khamala amesema inasikitisha wanasiasa kutumia hafla za matanga kuzua ghasia na hata kuachia familia hasara ya ubomozi wa vifaa na viti ambavyo vimekombolea

“Mimi ntaambia wachungaji kufungia wasiasa wasiongee kwa matanga kwasababu hao si waukoo wa hiyo boma na wanaleta fujo na kuvunja viti hema na kusababisha hasara kubwa na nawahimiza wachungaji muweze kuzingatia hayo.” askofu khamala alisema

Mwakilishi wa akina mama kaunti ya Kakamega Elsie Muhanda amewataka akina mama kuwalea watoto na kuwakubalia wasichana wao ambao walipachikwa mimba kurudi shule akiwasuta wale ambao wanawahangaisha watoto wao na kukataa kulea watoto

mama Elsie akiieleza “Kupata mimba ya kwanza sio kosa kurudia ndio kosa. Wazazi Fulani mmeficha watoto kwa nyumba muwaruhusu waende shule na wale wamejifungua wazazi muwalinde watoto wao ili waweze kurundi shule kwasababu wamepewa hiyo nafasi ya kurudi shule”

 Mwakilishi wadi hiyo ya Butsotso ya kati Lyston ambundo kwa upande wake amewahimiza wakazi kuunga mkono ripoti ya BBI kutoa fursa ya raslimali kuteremshwa hadi kwenye wadi

“Ikiwa tutapewa kama milioni 20 na tuongezewa kama milioni 6 na wabunge wakifanya kazi kubwa pia sisi MCA apa chini tunawasaidia tutaendelea mashinani”

Story by Boaz Shitemi

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE