Seneta mteule kutoka kaunti ya Kakamega Naomi Shiyonga amewarai wakazi wa Matungu kujitokeza kwa wingi tarehe 4 mwezi ujao kushiriki uchaguzi mdogo utakaofanyika ili kumchagua mbunge wao baada ya aliyekuwa mbunge wa eneo hilo Justus Murunga kufariki.
Akizungumza baada ya kuvitembelea vikundi vya akina mama kwenye wadi ya Namberekeya Shiyonga amewataka wakazi hao kujitokeza kwa wingi ili kumchagua kiongozi atakaye wafanyia maendeleo kwa muda uliosalia.
Shiyonga aidha amempigia debe David Were anayewania kiti cha ubunge kupitia chama cha ODM akisema kuwa Wanamatungu wanafaa kumchagua kiongozi atakayewafanyia maendeleo kwa kuimarisha miundo msingi eneo hili.
Kwa upande mwengine amewarai wanasiasa wanaowania kiti hicho kufanya kampeni za amani bila kuchochea vijana na wafuasi wao kuzua vurugu kwenye mikutano ya wapinzani wao.
Story by James Shitemi