Baadhi ya viongozi wa kisiasa na wafanyabiashara kutoka kaunti ya Vihiga wamemtaka kinara wa chama cha ODM Raila Odinga kuunga mkono juhudi za kinara wa ANC Musalia Mudavadi za kutaka kuliongoza taifa
Wakiongozwa na Harun Mshivoji wanasema kuwa Raila amekuwa akipata uungwaji mkono wa jamii ya mulembe kwa muda mrefu na sasa wakati umewadia wa yeye kurudisha mkono; huku wakimuonya Mudavadi dhidi ya kushirikiana na Raila iwapo Raila ndiye atakaye peperusha bendera ya urais tena mwaka ujao
Viongozi hao aidha wamemkashifu Raila kwa kuisahau jamii ya mulembe kimaendeleo licha ya wao kusimama naye kwenye azma zake
By Richard Milimu