Shule ya upili ya wavulana ya St Lukes Kimilili iliyo katika eneobunge la  Kimilili imefungwa kwa muda usiojulikana na wanafunzi kutumwa nyumbani kwa likizo ya lazima baada yao kugoma na kuharibu mali  shuleni humo usiku wa kuamkia leo huku kisa hiki kikijiri siku moja tu baada ya shule ya upili ya wavulana ya Chesamisi kufungwa hapo jana kufwatia utovu wa nidhamu miongoni mwa wanafunzi.

Akitoa uamuzi shuleni humo Mkurugenzi wa Elimu kaunti ya Bungoma Philip Chirchir amesema hatua hiyo imeafikiwa baada ya bodi ya shule hiyo kutathmini uharibifu uliosababishwa na wanafunzi hao kando na kuwepo taharuki miongoni mwao.

Kwa upande wake mwalimu mkuu wa shule hiyo Innocent Siro amethibitishwa kuwa wanafunzi wote wako salama hata baada ya rabsha hiyo kuzuka.

Hata hivyo naibu kamishna wa Kimilili Kiplagat Tarus amedokeza kuwa tayari uchunguzi umeanzishwa kubaini chanzo cha mgomo huko akihoji kuwa yeyote atakayepatikana kuhusika atachukuliwa hatua kali za kisheria huku akiarifu kuwa matumizi ya mihadarati huenda ilichagia utovu huo wa nidhamu.

Story by Richard Milimu

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE