Mkufunzi mkuu wa timu ya raga ya Kabras Mzingaye Nyathi ameanzisha mchakato wa kuimarisha timu hiyo mbele ya kuanza kwa ligi kuu ya mchezo huo almaarufu kama (kenya cup) ambayo inatarajiwa kuanza rasmi mwisho wa mwizi huu
Akizungumza muda mfupi tu baada ya uzinduzi rasmi wa jezi mpya ya timu hiyo katika uwanja wa maonyesho ya Kakamega kocha huyo ambaye ni raia wa Zimbabwe amefichua kuwa ujio wa korona nchini ulisambaratisha juhudi za timu hiyo ambayo ilikuwa inalenga kutwaa ubingwa wa kombe hilo huku akiwakikishia mashabiki kwamba watafanya kila wawezalo kushinda mechi zao
Kwa upande wao wachezaji wamelezea kujitolea kwa o kuhakikisha kwamba juhudi zao zinazaa matunda na lengo kuu likiwa kushinda kombe la kenya cup huku wakimshukru mfadhili wao kwa kusimama nao kwa kipindi chote tangu mlipuko wa korona
Timu hiyo ya kabras itachuana na kenya harlequins wikendi hii kwa kombe la charity cup kabla ya kuanza rasmi michuano ya kenya cup na timu mmust mnamo tarehe 27 mwezi huu
Story by Richard Milimu