Tume ya Huduma za Walimu, TSC imetangaza rasmi nafasi elfu moja za kuwapandisha vyeo walimu kuanzia Februari mwezi ujao.

TSC inalenga kuwapandisha vyeo walimu mia nne tisini na wawili wa shule za upili walio chini ya kitengo cha kwanza cha kazi T-scale 8.

Aidha walimu wengine ni mia tatu sitini na watatu wa kitengo cha nne cha kazi T-scale 9.

Tume hiyo vile vile,  imetangaza kuwapandisha vyeo walimu sabini na wawili kuwa manaibu walimu wakuu na wengine kumi na watano kuwa walimu wakuu huku ishirini na wanane wakiwa wahadhiri wakuu.

Afisa Mkuu Mtendaji waTSC, Nancy Macharia amewashauri walimu wanaolenga kupandishwa vyeo kutuma maombi kuambatana mwongozo wa maendeleo ya taalumu ya ualimu.

Story by Stacy Achieng

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE