LUBAO FREQUENCY MODULATION LIMITED

Uniting Communities
  1. Listen to Lubao FM Live 102.2 FM

Live now:

Up next:

Uchaguzi Sokoni Shinyalu

Wafanya biashara wa soko la shinyalu lililo katika wadi ya isukha ya kati eneo bunge la shinyalu kaunti ya kakamega , wameshiriki kwenye uchaguzi wa viongozi wa soko hilo ijuma ya leo

Uchaguzi huo umefanyika kwa njia ya amani na kuwashirikisha wagombea watatu kwenye wadhifa ya mwenye kiti ambao ni; bw. Patrick afwayi makolo, bw. Titus kachitsa shivanda na bw.henry amwoka isabwa ambaye alikuwa akitetea kiti hicho kwa mara ya pili na kuibuka mshindi kwa kujizolea kura 212 akifwatiwa na patrick – kura 42 naye titus akiwa wa tatu na kura 18.

Bw. Amwoka amewapongeza wapiga kura na kuwaahidi kufanya kazi na kuimarisha soko hilo.

Kwenye nyadhifa zingine, naibu mwenye kiti wa akina mama bi florence shicheyi, mwakilishi wa akina mama bi roselidah shinali, kiongozi wa vijana bw. Allan simbole, mweka hazina bi. Rosalia mushila, na kiongozi wa walemavu bw. Benard mwori walipita bila kupingwa na kuwashukuru wapiga kura.

Bw. Amwoka amepongezwa na wafanya biashara na kumtakia kila la heri.

by sajida wycliffe

Charles Oduor

Read Previous

Madereva wa trela wahangaishwa na KENHA mjini Eldoret

Read Next

KATIBU MKUU WA ELIMU KUZURU KAUNTI YA UASIN GISHU

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *