Uchaguzi wa bodi ya wasimamizi kwenye hospitali ya Shikusa lokesheni  ndogo ya Lubao wadi ya Isukha kazkazini eneo bunge la Shinyalu kaunti ya Kakamega umeandaliwa leo huku wakaazi tokea lokesheni ndogo ya Lubao wakishiriki kwenye zoezi la upigaji kura chini ya utawala wa eneo hilo likiongozwa na naibu chifu Sulvei Shiafu

Kwenye matokeo ya uchaguzi huo Gaitano Milimu amechaguliwa kama mwenyekiti wa bodi hiyo kwa kujizolea kura 19 na kumshinda mpinzani wake Albert Milimu aliyejizolea kura 10

Kwenye wakilishi wa kina mama kwenye bodi hiyo Joan Litsalia amechaguliwa kwa kura 15 na kuwashinda wapinzani wake Rebecca Nasiche aliyejizolea kura 11 naye Truphena Ashiono akijizolea kura 1

Katika nafasi ya uwakilishi wa vijana kwenye bodi hiyo Mwera Ashlima Mwera ameshinda uchaguzi huo na kujizolea kura 15 huku Anthony Shihundu Imbani na Dennis Lanya wakijizolea kura 6 kila mmoja huku Jackline Luvanga akijizolea kura 1

Naibu chifu wa lokesheni ndogo ya Lubao Sulvei Shiafu amewapongeza wawakilishi waliochaguliwa na kuwatakia kila la heri kwenye kazi yao huku akitaka jamii kushirikiana nao ili kuendeleza huduma nzuri za hospitali hiyo ya Shikusa na kuwataka wanainchi kutumia vyema hospitali ya Shikusa ili kupokea matibabu na kuepukana na maafa zaidi

Nayo kamati inayoondoka chini ya mwenyekiti Josphat Muchiti na mwakilishi wa kina mama Rosemary Musila imeshukuru ushirikiano uliokuwepo baina ya hospitali hiyo na bodi ya jamii iliyokuwa inawakilisha matakwa ya wakaazi wa sehemu hiyo wakipongeza viongozi waliochaguliwa kwa kuwatakia kila la heri huku wakitoa changamoto kwao kueneza jumbe nzuri kuhusiana na hospitali hiyo huku wakiwataka kujitolea muhanga na  kusaidia hospitali ya Shikusa

By Sajida Javan

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE