Wakazi kutoka kijiji cha Eshisiru eneo bunge la Lurambi kaunti ya Kakamega wamelalamikia ongezeko la visa vya uhalifu katika eneo hilo huku wakiwashtumu maafisa wa usalama wanaohudumu katika eneo hilo kwa madai ya utepetevu. 

Wakazi hao wamelalamikia kisa ambapo mlinzi mmoja aliuawa usiku wa kuamkia jana na watu wasiojulikana akiwa kazini katika kituo cha kibiashara cha Eshisiru.

Sasa wanawataka maafisa husika wa usalama kuwajibika kwa kuimarisha doria hasa nyakati za usiku ili kuthibiti visa vya utovu wa usalama ambavyo vimekithiri eneo hilo.

By Javan Sajida

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE