Wizi mjini Lubao umekidhiri kiasi kua wiki halipiti kabla ya kuripotiwa tendo la kuibiwa haswa kwa wafanyibiashira ambao katika juhudi zao za kujiimarisha na kujenga uchumi wa taifa letu wanajipata mikononi mwa vijana wanaozishambulia biashara zao usiku na kuwaibia huku wakilemaza jitahada zao za kujiendeleza.
Katika kisa cha hivi leo, Hamisi Ngasi anasema kua duka lake la mbao lilibomolewa usiku wa kuamkia leo na watu wasiojulikana wakatoweka na vifaa vyake vya kazi.
Akidai kua hii ni mara yake ya pili mwaka huu kuibiwa katika duka lake, ametoa wito kwa maafisa wa polisi katika eneo hili kuwajibika ili kumsaidia kurejelea biashara yake.
Kwa upande wake, mzee wa kijiji cha sokoni, Lubao Sisiko Seyi Wakukha ametoa wito kwa vijana kutafuta njia mbadala ya kujikimu kimaisha. Vile vile aliwaonya vijana dhidi ya kukiuka masharti ya kutotoka nje yaliyowekwa na serikali akidai kua watajipata taabani.
Kisa hicho kimedhibitishwa na polisi mjini Lubao ambao wameanzisha uchunguzi.
Wycliffe Andabwa