Wafanyibiashara sokoni Makunga eneobunge la Mumias Mashariki wanalalamikia ukosefu wa maji sokoni humo
Wafanyibiashara hao sasa wanahofia mkurupuko wa Magonjwa kutokana na tatizo hilo
Vilevile amesikitikia mazingira duni wanamoendeshea biashara zao huku taka zikijaa kote sokoni
Wafanyibiashara hao aidha hutatizika haswa masaa ya jioni baada ya taa ilowekwa pale na serikali ya kaunti ya Kakamega kufeli kufanya kazi siku kadhaa zilizopita
Sasa wanaitaka serikali ya kaunti ya kakamega kuingilia kati na kutatua tatizo hilo ikitiliwa mkazo ushuru wa juu wanaotozwa
Haya yanajiri siku chache tu baada ya nyuki amabao wamehamia sokoni humo kuwafurusha sokoni humo huku wakimvamia na kumjeruhi vibaya mojawapo wa wafanyibiashara wa soko hilo
By James Nadwa