Kuna haja ya kustawisha na kukuza utamadumi wetu ili kuunganisha jamii zetu. Haya yalisemwa na makamu mkuu wa chuo kikuu cha sayansi na teknolojia, prof. Simon shibairo alipokua akifungua rasmi sherehe za utamaduni katika chuo hicho.huku akizungumzia kuhusu tamaduni kwenye shule hiyo
Wanafunzi wametoka sehemu tofauti tofauti na wanakutana hapa chuoni na kile ambacho huwaleta pamoja ni masomo lakini kando na masomo pia tunawapa nafasi ya kuweza kuomyesha utamaduni wao kutoka sehemu ambazo wamelelewa na hapo tunajifunza tamaduni na tunaweza kuwaheshimu kabila zote kwa maana tumeweza kujifunza utamaduni wao na kuelewa. Vile vile kupitia kwa siku ya utamaduni tunaeza kushi kama jamii moja na pia kukuza mazingara kulingana na utamaduni wetu
Pia alizungumzia kuhusu talanta ambazo ziko miongoni mwa vijana katika chuo hicho na wanavyo zionyesha siku ya chuo kinapo adhimisha utamaduni na huwa wanaangazia wanafunzi bora katika utamaduni na hupewa uthamini na chuo hicho.
Wanafunzi wengi katika hiki chuo wanatalanta mbalimbali na talanta zao kwa mira mingi huwa wanaonyesha wakati wa utamaduni . Kama chuo huwa tunaangalia talanta ya wanafunzi na wanapewa talent scholaship maana kuwa tunakuza ile talanta mwanafunzi ako nayo na vilevile anaendelea na masomo yake pale chuoni
Vilevile pia amewapa tumaini wanannchi kuhusiana na janga la corona na pia kuwahimiza wanafunzi kuendelea kuzingatia maagizo ya afya wakati wanapo sherekea utamaduni wao
Tunamshukuru mungu kwa umbali ametutoa na kutulinda kwa maana bila yeye hili janga la korona lingekua limetumaliza kitambo. Kwa sasa tumejua jinzi ya kujilinda kutokana na corona na pia imune yetu ikiwa very strong najua tutashinda corona na itaisha kabisa.
By Lihavi Imelda