Aliyekuwa kwa wakati mmoja mjumbe wa Funyula Paul Otuma sasa ameusuta uongozi wa kaunti ya Busia kwa kukosa maono ya maendeleo kwa kaunti hiyo.
Akiwa katika eneo ya Malanga eneo bunge la Nambale Otuma amesema kuwakulingana na takrimu za hivi punde kaunti ya Busia imeorodheshwa miongoni mwa kaunti maskini nchini licha ya kupakana na nchi jirani ya Uganda.
Otuoma amesema kuwa kwa saa hizi kaunti ya Busia inahitaji uongozi utakaoboresha miundo misingi na sekta ya afya huku akihoji kuwa hilo litafanyika tu kama uongozi wa sasa utabadilishwa wakati wa uchaguzi mkuu mwakani.
Ikumbukwe kwamba gavana wa sasa wa kaunti ya Busia Sospetr Oojamong ameonekana kumpikia upato naibu wake Peter Mulomi huku akisema kuwa chini ya uongozi wake kama gavana wa Busia kila mwananchi wa Busia ana kila sababu ya kutabasamu huku akisema kuwa ikiwa Mulomi atamridhi Busia itakuwa mahali pa kujivunia hata zaidi swala ambalo Otuoma amelitaja kama kejeli kubwa kwa wenyeji wa Busia.
By Hillary Karungani