Kundi moja la vijana kutoka eneo bunge la Matungu kaunti ya Kakamega limeanzisha kampeini ya kuwasajili vijana nyumba kwa nyumba kama wapiga kura kabla ya uchaguzi mkuu ujao.

Wakiongozwa na Donald Okumu vijana hao wanasema wameamua kuanzisha mpango na lengo la kuhakikisha vijana waliohitimu miaka 18 wanapata vitambulisho vya kitaifa sawa na kuwashawishi kuchukua kadi ya kura kabla ya uchaguzi mkuu ujao.

Aidha wameshauri vijana kote nchini kujitenga na wanasiasa wachochezi hasa taifa hili linapojiandaa kwa uchaguzi mkuu wakitoa wito kwa tume uwiano na utangamano kunoa makali yake wakati huu siasa zinapokaribia kunoga.

By Lindah Adhiambo

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE