Siku moja baada ya mtu mmoja kuonekana kwenye mitandao za kijamii akijaribu kusimamisha  gari alimokuwa ndani Rais Uhuru Kenyatta kwenye msafara wake , sasa mbunge wa Lurambi askofu Titus Khamala amemtaka Rais kuwaruhusu  watu wa aina hiyo kumwelezea shida zinazowakumba badala ya maafisa wa usalama kuwazuilia.

Akizungumza baada ya kuzindua ujenzi wa madarasa manane ya gorofa katika shule ya upili ya Shieywe mjini Kakamega Khamala anasema kuwa haoni kama mwanaume huyo alikuwa na nia ya kutishia usalama wa rais akihoji kuwa anachojua  wakenya wengi wanakumbwa na umaskini mwingi ukiwemo ukosefu wa ajira na huenda ndio moja ya sababu kuu ya mwanaume huyo kutaka kumuona Rais Kenyatta.

Kulingana na askofu Khamala anataka Rais Uhuru kuhiga mfano wa aliyekuwa rais wa Tanzania hayati John Pomby Magufuli na marais wengine ambao hukubalia wananchi walio na matatizo kutoa hisia zao wakati anapozuru eneo lolote ya nchi.

By Linda Adhiambo

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE