Baadhi ya vyongozi pamoja na wakaazi wa mtaa wa Makunga wilayani Mumias Mashariki sasa wanataka usimamizi wa hospitali ya Makunga kubadilishwa kama njia pekee ya kuboreshewa kwa huduma katika kituo hicho Cha afya
Wakiongozwa na Caleb Okumu mwenyekiti wa wanabodaboda Makunga Corner Stage vyongozi hao wanausuta uongozi wa hospitali hiyo kwa utepeteveu
Wale wasimamizi wa hospitali wabadilishwe kwa sababu wagojwa kwa mara mingi wanasaidiwa tu na watchman hasa sana mama wajawazito
Wakaazi hao aidha wametaja baadhi ya vifo vya wagonjwa kikiwemo Cha hivi punde Cha mhasiriwa wa ajali wiki iliyopita wakivihusisha na uzembe kwenye usimamizi wa hospitali hiyo
Wagojwa hawaudumiwi na wanakufa bila ata kushughulikiwa. hata kama akuna matibabu ya kutosha ni vizuri hospitali kuelekeza mgojwa katika hospitali nyingine
.Wakaazi hao wamedokeza kuwa wagonjwa pamoja na wafanyikazi wa hospitali hiyo hukumbana na masahibu ya yakiwemo kunyimwa chakula huku usimamizi ukisalia kimya kuhusu swala hilo
Juhudi zetu za kuzungumza na wakuu wa hospitali hiyo ya Makunga hazikufua dafu baada ya afisa anayesimamia kituo hicho kudinda kuzungumzia swala hilo
By James Nadwa