Pendekezo la kurejesha adhabu ya kiboko shuleni linaonekana kuwavutia baadhi ya wazazi huku wakisema kwamba itasaidia kumaliza visa vya utovu wa nidhamu kwa mwanafunzi.
Kwa upande wake bwana Isaac Taly mkaazi wa Buyangu katika wadi ya Isukha Kaskazini kaunti ya Kakamega, anasema kwamba lawama kubwa inamwelekea mzazi kwa kumdekeza mwanaye na kumpandika jina huku akijiona ametosha.
Hata hivyo naye bwana Patrick Mutsami anafichua kwamba mzazi hakuchukua jukumu lake alipokuwa na mwanaye nyumbani wakati wa likizo refu ya kipindi cha covid-19 na kuunga mkono kurejeza adhabu ya kiboko shuleni
Story by Sajida Wycliffe