Kati ya vijana 329 waliojitokeza kushiriki zoezi la kuwasajili vijana kujiunga na kikosi cha polisi lililofanyika katika shule ya msingi ya Isanjiro ilioko mjini Malava vijana 14 peke ndio ambao wamefuzu na kuruhusiwa kujiunga na kikosi hicho.
Akizungumza na wanahabari baada ya kukamilisha zoezi hilo Afisa msimamizi Peter Malinge amehoji kuwa hakuna kisa chechote kibaya kilichotokea wakati wa hafla hiyo.
Aidha Malinge amewarai vijana ambao hawajafusu kujiunga na kikosi hicho kuendelea kujaribu bahati katika zoezi lingine ili wapate nafasi na kutimiza ndoto yao.
Hata hivyo vijana waliokosa nafasi hiyo hawajafuraishwa na jinsi zoezi hilo lilivyoendeshwa wakidai kuwa stakabadhi walizoitishwa za kuonyesha maisha yao ali maarufu good conduct haikuwa imetoka.